
Jinsi MGL Africa inavyotunza taarifa zako kwenye tovuti hii, duka la mtandaoni na app ya MGL Africa.
Imesasishwa: 13 Oktoba 2026
MGL Africa (Masha Global Link Co. Ltd) inaagiza bidhaa kutoka China kuja Tanzania na kuuza bidhaa zilizopo Tanzania. Sera hii inahusu mglafrica.com, store.mglafrica.com na app ya MGL Africa.
Jina lako, namba ya simu, barua pepe (ukitupa), namba ya WhatsApp na anwani za kupokelea mzigo. Oda zako, bidhaa zilizomo, malipo na risiti, nukuu za bei na ankara, na ufuatiliaji wa mzigo wako. Maoni na ujumbe unaotutumia. Taarifa za kiufundi zinazohitajika kukuweka ndani ya akaunti (tokeni ya kuingia kwenye simu yako). App haitumii eneo ulipo, kamera, namba za simu ulizohifadhi wala maikrofoni.
Kukufungulia akaunti na kukuingiza, kupokea na kukufikishia oda zako, kununua bidhaa zako kwa wasambazaji, kuzisafirisha na kuzitoa bandarini, kupokea malipo yako na kukupa risiti na ankara, kukutumia taarifa za oda kwa SMS, WhatsApp au barua pepe, na kujibu maswali yako. Pia tunatunza kumbukumbu za mauzo na malipo kwa sababu sheria za kodi za Tanzania zinataka hivyo.
Malipo hufanyika kwa pesa za simu, uhamisho wa benki au kampuni ya malipo. Tunarekodi kiasi, njia ya malipo na namba ya muamala. Hatuoni wala hatuhifadhi namba ya kadi yako au PIN ya pesa za simu.
Kila mmoja anapata kile anachohitaji tu: kampuni za malipo kupokea malipo yako, watoa huduma za SMS na WhatsApp kukutumia taarifa, wasambazaji wetu, mawakala wa usafirishaji na forodha na wasambazaji wa mizigo kununua, kusafirisha na kukufikishia bidhaa zako, na mamlaka za serikali pale sheria inapotaka. Hatuuzi taarifa zako.
Taarifa za akaunti yako zinatunzwa ukiwa na akaunti. Ukiifuta, jina lako, simu, barua pepe na anwani zinafutwa. Oda, ankara na malipo zinabaki bila taarifa zako binafsi kwa muda ambao sheria za kodi za Tanzania zinataka.
Unaweza kuona na kurekebisha taarifa zako kwenye app au dukani (Akaunti), kuzima taarifa za SMS, WhatsApp au barua pepe, na kufuta akaunti yako wakati wowote. Pia unaweza kutuuliza tunatunza taarifa gani kuhusu wewe.
Maswali kuhusu taarifa zako: tumia ukurasa wa Wasiliana nasi, au namba ya simu na anwani zilizo chini ya kila ukurasa.
Unataka kufuta akaunti yako? Angalia jinsi ya kufuta akaunti.